A+ Kiswahili KCSE: Marudio ni kitabu cha marudio kinacholenga watahiniwa wa
KCSE. Kitabu hiki kimeandikwa kwa mtindo wa maswali na majibu kwa kuzingatia
mada zote zinazotahiniwa kulingana na mtaala wa KCSE.
Sifa kuu bainifu zinazokifanya kitabu hiki kuwa mwimo wa mwanafunziÂ
anayetarajia kupata alama ya A+ katika mtihani wa KCSE-somo la Kiswahili niÂ
kama zifuatazo:
Maswali na majibu ya papo kwa Napo kulingana na mpangilio wa mtihani wa Kiswahili, ngazi ya KCSE.
Maswali kabambe na majibu ya karatasi ya kwanza: 102/1; insha. Insha zote zinazotahiniwa kulingana na silabasi zimetotewa maswali na majibu
Maswali na majibu ya karatasi ya 102/2; matumizi ya lugha na isimujamii  ambapo maswali na majibu ya vipengee vifuatavyo yametolewa; ufahamu, ufupisho(muhtasari), matumizi ya lugha na isimujamii.
Maelezo na maelekezo ya jinsi ya kujibu maswali ya vipengele vyote ili mwanafunzi afahamu jinsi anavyoweza kupata alama za juu
Vifungu vyenye mada za masuala ibuka iii kwenda na wakati na kuwapa wanafunzi stadi bora za maisha kando na kupita mtihani wa KCSE
Lugha nyepesi isiyokanganya katika kujibu maswali wakati wa marudio
Mwongozo wa usahihishaji wa maswali ya karatasi mbalimbali(insha,ufahamu, ufupisho, matumizi ya lugha na isimujamii)